Mahafali Ya Shule Ya Sekondari Ya Wasichana Ursuline- Njombe – Nyombo 2021

Mahafali Ya Kwanza

Picha ya pamoja wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa na mgeni rasmi (wa tatu kutoka kushoto), meneja wa shule (wa nne kutoka kushoto), mkuu wa shule (wa pili kutoka kushoto na wajumbe wa bodi ya shule)

Mnamo tarehe 18/09/2021 shule ya sekondari ya wasichana Ursuline inayomilikiwa na masista wa shirika la Mtakatifu Ursula wa Maria Imakulata, ilifanya mahafali yake ya kwanza ya kidato cha nne yakiongozwa na mgeni rasmi Mama Pindi Chana mbunge wa viti maalumu . Katika mahafali haya wanafunzi 27 wasichana walihitimu. Mahafali hayo yalifana sana yakipamba na michezo mbalimbali toka kwa wahitimu na wanafunzi wengine.

Picha ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiwa wanatoa ngonjera wakielezea historia ya shule yetu.

Mgeni rasmi amewahimiza sana wahitimu kutumia vyema muda wao uliobaki katika kujiandaa vyema kufanya mtihani wao wa kidato cha nne kwani kwa kufanya hivyo watapata matokeo yenye tija. Aidha amewapongeza sana wamiliki wa shule yetu hii kwa jitihada na majitoleo yao ya kuanzisha shule katika kijiji hiki cha Nyombo mkoani Njombe.

Baadhi ya wanahitimu wa kidato cha nne mwaka 2021

Amewasisitizia sana kuendelea kutumia ujuzi walio nao katika kuboresha taaluma na nidhamu ya wanafunzi. Shule ilimzawadia mgeni rasm zawadi kwa ukarimu wake na upendo wake kwetu kwa kutumia muda wake wa ziada kuja na kuipamba siku hiyo. Naye mgeni rasm aliahidi zawadi yake kwa shule kama alama ya mchango wake katika huduma zinazotolewa.

Wanafunzi walitunukiwa vyeti vyao ikiwa ni alama ya ushindi katika safari ndefu ya mafanikio yao. Wahitimu wetu walijawa na furaha kubwa pale walipopewa zawadi hii ya ushindi ikiwa ni ishara ya mafanikio huko waendako.

kama huwezi kupaa, kimbia, kama huwezi kimbia, tembea na kama huwezi tembea basi tambaa, hii yote iwe ni kufikia lile lengo ulilojiwekea.

by Martin Luther the King.

Uongozi wa shule unapenda kuwakaribisha kwa maoni yoyote ili kukuza shule yetu. Kama umependa ujumbe usisite kutuandika katika comment section hapo chini. Asante

Similar Posts

One Comment

  1. Hongera sana kwa juhudi ya mapambano ya kuwapatia elimu watoto wetu hasa wa kike. Mungu azidi kuwastawisha na kuwabariki zaidi.
    Tupo pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *