|

Mahafali Ya Shule Ya Sekondari Ya Wasichana Ursuline- Njombe – Nyombo- 2022

MAHAFALI YA PILI

wahitimu wetu wa mwaka 2022

Mahafali haya yamefanyika mnamo tarehe 10/09/2022 yakipambwa kwa uzuri kabisa na mheshimiwa mama Joyce Mayemba . Mahafali yalianza kwa ibada takatifu ya misa iliyoongozwa na mheshimiwa Padre Edward Msigwa paroko wa parokia ya Matembwe.

Huu ndiyo mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu
Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi

Baada ya ibada bendi ya shule ilijiandaa kikamilifu tayari kumpokea mgeni rasmi kwa ajili ya kuanza rasmi mahafali yetu

bendi ya shule
Mbele ya geti la shule

Bendi ya shule imesimama kwa ukakamavu mkubwa tayari kumpokea mgeni rasmi kwa ajili ya kuanza mahafaliyetu ya leo rasmi.

Ratiba mbalimbali ziliendelea katika ukumbi wa mahafali bila kukomasa maburudisho mbalimbali kama vile;

wanafunzi wakicheza ngoma ya kitamaduni
mwanafunzi wa kidato cha kwanza akisema mistari ya biblia kwa lugha ya kingereza
wanafunzi wa kidato cha kwanza wakisema historia ya shule kwa lugha ya kingereza kwa mtindo wa
ngonjera
wanafunzi wakitoa igizo lenye kuelimisha vijana juu ya kuwa na msimamo katika maisha yao

sherehe iliimmalizika kwa shamrashamra nyingi kabisa ikiwa ni kiashirio kwamba siku ilikuw njema machoni pa Bwana.

Uongozi wa shule unapenda kuwakaribisha kwa maoni yoyote ili kukuza shule yetu. Usisite kutuandika chochote katika comment section hapo chini. Aksanteni sana na karibu URSULINE GIRLS SECONDARY SCHOOL kwa malezi bora ya mtoto wa kike.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *